IQNA

Watetezi wa Palestina

FBI yashtakiwa kuhusu  orodha ya kufuatilia wanaounga mkono Palestina

16:21 - August 13, 2024
Habari ID: 3479272
IQNA - Kundi la kutetea haki za Waislamu Marekani limetangaza kesi dhidi ya serikali ya shirikisho kwa kuwaweka Wapalestina-Wamarekani wawili kwenye orodha ya siri ya kufuatiliwa kutokana na msimamo wao wa kuwaunga mkono Wapalestina wanaoteswa na Israel huko Gaza.

Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani (CAIR) kupitia tawi lake la Greater Los Angeles Area (CAIR-LA) limefungua kesi hiyo dhidi ya Shirika la Upelelelzi la Marekani (FBI) mahakamani.

Kesi hiyo inasema serikali ilimweka Mpalestina-Mmarekani mmoja kwenye Orodha ya No Fly, yaani kuzuiwa kusafiri kwa ndege' na kukamata kifaa cha kielektroniki cha mwingine wakati ikimhoji kuhusu harakati zake halali.

Kwa mujibu wa CAIR, Dk. Osama Abu Irshaid na Bw. Mustafa Zeidan, wote raia wa Marekani wenye asili ya Palestina, wamekuwa wakizuiliwa na kuhojiwa.

Irshaid ameripotiwa kuzuiliwa mpakani mara kadhaa, wakati ambapo maajenti wa FBI walimkamata simu na kumuhoji kuhusu vyama na kazi yake.

"Jambo moja tu limebadilika kwa Dk. Abu Irshaid katika miezi ya hivi karibuni: utetezi wake wa mara kwa mara na wa shauku wa kukomesha mauaji ya kimbari ya Israeli huko Gaza na kukomesha ushiriki wa Marekani katika mauaji hayo," inasomeka kesi hiyo.

Zeidan, ambaye pia "huandaa maandamano ya kila wiki ya kutaka kusitishwa kwa kampeni ya mauaji ya halaiki ya Israel huko Gaza," alizuiwa kupanda ndege kuelekea Jordan kumtembelea mama yake mgonjwa bila maelezo, kulingana na kesi hiyo.

CAIR inasema kuwa hatua hizi si kwa madhumuni ya usalama lakini badala yake zinalenga watu binafsi kwa utekelezaji wao halali wa haki za kikatiba.

Shirika hilo limepokea ripoti kutoka kwa Wamarekani ambao wamekabiliwa na unyanyasaji kutokana na harakati zao za kuunga mkono Palestina.

3489490

Habari zinazohusiana
Kishikizo: cair palestina marekani
captcha